Thursday, 15 July 2010

MAKULILO SCHOLARSHIP BLOG YATIMIZA MIAKA 3

Libeneke La Nondozzz Latimiza Miaka Mitatu

Picha kushoto: Issa Michuzi (MICHUZI BLOG), Mrs. Marie A. Makulilo, Mr. Ernest B. Makulilo (MAKULILO BLOG)


MAKULILO SCHOLARSHIP BLOG
INAADHIMISHA MIAKA 3.
BLOG ilianza kufanya kazi rasmi kuanzia JULY 2007. Mwezi huu JULY 2010 ni mwezi wa maadhimisho. Nipo katika hatua za mwisho za maboresho ya BLOG hii ambapo nitaongeza kipengele cha SCHOLARSHIP AUDIOS/VIDEOS ambapo nitakua najibu maswali ya wadau na kuweka dondoo za maandalizi ya mtu kuweza kupata scholarships North America na Western Europe.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadau wote ambao wamekuwa katika mstari wa mbele kunisaidia katika mambo ya BLOG hususani MICHUZI (WWW.ISSAMICHUZI.BLOGSPOT.COM) na DA SUBI (WWW.WAVUTI.COM) . Pia nawashukuru wale wote walionisaidia kuweza kuongea ktk ITV, TBC1 na TBC TAIFA kuhakikisha watu wengi wanajua taratibu za uombaji scholarships ughaibuni.

Naomba maoni yenu katika kuwezesha maboresho ya BLOG hii. Pia natoa wito kwa wengi kujiunga na SCHOLARSHIP FORUM WWW.SCHOLARSHIPNETWORK.NING.COM

ambapo unatakiwa ku-SIGN UP na kuwa member. Mara uwapo member utakuwa unapata scholarship updates kwenye E-MAIL INBOX yako kila ninapoweka taarifa kwenye FORUM na utakuwa na nafasi ya kuweka comment au kuuliza swali na kujibiwa papo hapo.

No comments:

Post a Comment

Girls Generation - Korean